Welcome to ED (Swahili)
Karibu katika ED
Wanju wanju, nidja
Tunawatambua watu wa Whadjuk wa taifa la Noongar, wamiliki wa jadi wa ardhi ambayo wapo kwa sasa na tunatoa heshima zetu kwa Wazee wa zamani na wa sasa.
Hospitali ya watoto ya Perth pia inaitwa PCH. Idara ya Dharura pia huitwa ED.
Tuko hapa kumsaidia mtoto wako kupata matunzo anayohitaji.
Tunawahudumia watoto walio na umri wa miaka 15 au chini kwa kuwapa huduma za dharura za matibabu au afya ya akili. Huduma hizi ni za bila malipo kwa raia au wakaazi wa Australia.
Muda wa huduma hizi unaweza kuongezwa hadi umri wa miaka 18, ikiwa wana hali ya kiafya iliyokuwepo kabla ya kuanza kwa huduma ambayo bado wanapokea huduma kwa ajili yake katika PCH na wamekuja ED wakiwa na hali hiyo hiyo.
Omba huduma za mkalimani ikiwa huelewi au ili kukusaidia kuzungumza nasi. Huduma hii ni ya bila malipo.
Muda wa kusubiri
Kunaweza kuwa na shughuli nyingi katika Idara ya Dharura hivyo kutakuwepo na watoto wengi wagonjwa wanaosubiri kuhudumiwa. Watoto walio wagonjwa zaidi huhudumiwa kwanza. Utaratibu na nyakati za kusubiri ziko sawa ikiwa utakuja kwa ambulensi. Unaweza kuangalia muda wa juu zaidi wa kusubiri kwenye skrini zilizo kwenye vyumba vya kusubiria.
Tafadhali tujulishe ikiwa unapanga kuondoka kabla hatujamtibu mtoto wako.
Shughuli zilizo katika Idara ya Dharura
Uchunguzi wa kwanza wa wagonjwa
Uchunguzi wa kwanza wa wagonjwa husaidia wafanyakazi kubaini uharaka wa mtoto wako kuonekana na daktari. Watamchunguza mtoto wako na kukuuliza maswali machache.
Kuingia Idara ya Dharura
Baada ya uchunguzi wa kwanza mtaingia ndani ya Idara ya Dharura na mtoto wako hadi kwenye ukumbi au chumba cha kusubiri. Karani atakuuliza maswali machache. Unaweza kusubiri kwa muda mfupi kabla ya kuhudumiwa na daktari. Tafadhali tujulishe ikiwa una wasiwasi kwamba hali ya mtoto wako inazidi kuwa mbaya.
Unaposubiri, ikiwa unaweza, fikiria kuhusu majibu yako kwa maswali yafuatayo.
Kwa nini umekuja na mtoto wako hospitalini leo?
|
- Je, hali hii imekuwepo kwa muda gani? Unafikiri ilisababishwa na nini? Je, wamewahi kuwa na hali kama hii hapo awali?
- Je, anahisi maumivu?
- Je, amekuwa akila/kunywa/kwenda chooni?
- Je, umemwona mtaalamu mwingine wa afya kwa tatizo hili?
- Je, kuna mtu mwingine amekuambia uje kwa ED?
- Je, amefanyiwa uchunguzi wowote au eksirei kabla ya kuja kwenye ED?
|
Je, historia ya matibabu ya mtoto wako ni ipi?
|
- Je, anapata huduma kutoka kwa mtaalamu wa afya kwa sasa? (Hii pia ni pamoja na huduma za afya ya akili)
- Je, ana hali au magonjwa gani mengine kwa sasa? (Kwa watoto wadogo, wafanyakazi wanaweza kuuliza kuhusu kuzaliwa kwao)
- Je, amekuwa na hali gaini magonjwa au upasuaji gani hapo awali?
- Je, amepokea chanjo zote anazostahili kupokea hadi sasa?
- Je, kuna historia yoyote ya hali au magonjwa katika familia ambayo ungependa kutwambia?
|
Mtoto wako anatumia dawa gani?
|
- Je, ametumia dawa gani katika siku chache zilizopita (ikiwa ni pamoja na antibayotiki)?
- Jina la dawa ni gani, dozi na anatumia mara ngapi kwa siku?
- Je, ni virutubisho gani, vitamini, au mitishamba ambayo mtoto wako amekunywa leo au anayotumia mara kwa mara?
- Je, hivi majuzi ameacha kutumia dawa zozote?
|
Mtoto wako ana mzio gani?
|
- Hii ni pamoja na mzio wa chakula, dawa, kuumwa na wadudu, na vitu kama vile lateksi au mavazi (hizi zinaweza kuwa zimethibitishwa au kushukiwa).
|
Je, kuna jambo lingine ambalo unafikiri tunapaswa kujua?
|
- Je, mtoto wako amepatwa na kiwewe chochote kinachohusiana na huduma za kiafya au matibabu?
- Je, wewe au mtoto wako mna mahitaji yoyote ya kitamaduni, kijamii, lugha, kifamilia au kitabia?
- Je, mara ya mwisho mtoto kula au kunywa kitu chochote ni lini?
|
Kuonana na muuguzi au daktari
Watauliza maswali na kuchunguza mtoto wako ili kutambua hali inayomkabili mtoto.
Unaweza kuomba kuzungumza na daktari kwa faragha bila mtoto wako kuwepo.
Vijana walio katika umri wa kubaleghe wanaweza kuomba kuzungumza na daktari/muuguzi kwa faragha bila mzazi wao kuwepo.
Mazungumzo kati yako na muuguzi au daktari wako
Daktari au muuguzi ataelezea hali inayoyomkabili mtoto na kile mtoto wako anachokihitaji.
Kuwa radhi kutuuliza maswali wakati wowote.
Vipimo na matibabu
Mtoto wako anaweza kuhitaji kufanyiwa kipimo cha damu, eksirei, au vipimo vingine ili kujua tatizo linalomsumbua. Wanaweza pia kupokea matibabu wakiwa katika ED. Huenda ukahitaji kusubiri matokeo ya vipimo au kusubiri kuona hali ya mtoto wako baada ya kupokea matibabu.
Kwenda nyumbani au kulazwa hospitalini
Kwa kutegemea na hali ya mtoto wako, utaweza kwenda nyumbani, kukaa kwa muda mrefu zaidi ili daktari wako aweze kufuatilia hali ya mtoto wako, au kulazwa hospitalini.
Kwenda nyumbani
Mtoto wako anapokuwa tayari kwenda nyumbani, daktari au muuguzi atakupa maelezo fulani kuhusu unachohitaji kufanya ili kumtunza mtoto wako, ambayo yanaweza kujumuisha laha ya maelezo kuhusu hali ya mtoto wako na barua kwa daktari wa eneo lako. Ikiwa wewe au mtoto wako mnahitaji cheti cha matibabu, tafadhali mwambie daktari au muuguzi wako kabla ya kuondoka. Kuwa radhi kutuuliza maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo.
Unapokuwa nyumbani, tafadhali fuata maagizo yoyote utakayopewa na daktari. Ikiwa una wasiwasi kuwa mtoto wako hapati nafuu, unaweza:
Kulazwa hospitalini
Mtoto wako anaweza kulazwa hospitalini kwa vipimo zaidi na/au matibabu chini ya timu ya Dharura au daktari mtaalamu wa hali fulani. Kusudi letu ni kutoa huduma karibu na nyumbani kwako, kwa hivyo tunaweza kumhamisha mtoto wako kwenye wodi ya watoto katika hospitali ya eneo lako kwa matibabu au wauguzi wa Hospitali ya Nyumbani (HiTH) wakutembelee ili kumpa utunzaji na kufuatilia hali ya mtoto wako.
Ikiwa unahitaji kukaa katika Hospitali ya Watoto ya Perth unaweza kuhamishwa hadi kwenye Kitengo chetu cha Kulazwa kwa Muda Mfupi (ESSU) au wodi ya hospitali.
Ikiwa mtoto wako atalazwa katika ESSU, atasalia chini ya uangalizi wa timu ya Dharura. Ikiwa mtoto wako anahitaji matibabu zaidi au upasuaji, atalazwa katika wodi ya hospitali.
Fahamu timu yako ya afya
Kuna watu wengi wanaohusika kumtunza mtoto wako.
Tuna Mhudumu wa Afya wa Asili (Aboriginal) anayepatikana siku nyingi za wiki ambaye atasaidia kutoa huduma ndani ya ED. Tafadhali omba kuwaona ikiwa ungependa.
Ikiwa unafikiria mtoto wako ana maumivu
Tafadhali zungumza na muuguzi ambaye atamtathmini mtoto wako na kumpa dawa ya maumivu inayofaa.
Una wasiwasi kwamba hali ya mtoto wako unazidi kuwa mbaya? Tunahitaji kujua
Ikiwa mtoto wako anaonekana kuwa mgonjwa zaidi au hali yake sio ya kawaida, tuambie mara moja. Unamjua mtoto wako vizuri zaidi. Tutakusikiliza.
Ikiwa huna uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiingereza vizuri, sema ‘Chumba cha Kusubiri cha Idara ya Dharura’ (Emergency Waiting Room)' au nambari ya chumba chako.
Maelekezo ya...
Vyoo
- Choo kinachoweza kufikiwa kwa urahisi ndani ya ED, upande wa kushoto wa mlango
- Kuelekea sehemu ya nyuma ya ED, karibu na chumba cha kungojea cha Pod C, nyuma ya sehemu ya kutengenezea Vinywaji
Tafadhali fuata mabango ya maelekezo au umuulize mfanyakazi ikiwa huna uhakika.
Chumba cha kubadilisha nepi za watoto
- Meza ya kubadilisha nepi iko ndani ya ED, karibu na choo, nyuma ya pazia la bluu
- Meza ya pili ya kubadilisha nepi iko katika mojawapo ya bafu karibu na Pod C
Maji ya kunywa
Maji yanapatikana katika Beverage Bay(Sehemu ya Kutengenezea Vinywaji) karibu na eneo la kusubiri la Pod C.
Chakula na vinywaji
- Vifaa vya kutengenezea chai na kahawa vya bila malipo viko katika Beverage Bay(Sehemu ya Vinywaji) ndani ya ED karibu na eneo la kusubiri la Pod C
- Mashine za kuuza vitafunio na vinywaji ziko nje ya ED karibu na lifti za Kijani
- Mgahawa wa Little Lion Cafe uko karibu na lango kuu kwenye Ghorofa ya Chini
- Eneo la Chakula (The Food Hall) liko kwenye Ghorofa 1, inaweza kufikiwa kwa lifti za rangi ya Waridi au ngazi zilizo nje ya Little Lion Cafe kwenye Ghorofa ya Chini
- A duka ndogo la vinywaji na vitafunio, Xpress Zone, iko kwenye Ghorofa ya Chini ya maegesho ya magari mengi ya QEII na inafunguliwa Jumatatu hadi Jumamosi, saa 7 asubuhi hadi saa 8 jioni.
Simu za umma za kulipia
Ziko nje ya ED kwenye korido inayounganisha ED na hospitali.
ATM
Iko nje ya ED kwenye korido inayounganisha ED na hospitali.
Usalama
Usalama wako ni muhimu sana kwetu. Ukiona tabia yoyote ambayo inakupa wasiwasi, au unahisi inaweza kuathiri usalama wako na wa mtoto wako, tafadhali wasiliana na mfanyakazi wa Usalama wa PCH kupitia 6456 3003 mara moja.
Haturuhusu unyanyasaji wa aina yoyote
Ili kuhakikisha usalama wa kila mtu, tuna sera ya kuzuia unyanyasaji na fujo.
Mtu yeyote anayehusika na unyanyasaji wa kimwili au wa matusi au fujo ataombwa kuondoka mara moja na walinda usalama wataitwa ikiwa itahitajika.
Kupiga picha na kurekodi video
Kwa ajili ya faragha na usiri wa wagonjwa, familia, watunzaji na wafanyakazi wetu, tafadhali usipige picha au kurekodi video ukiwa kwenye PCH.
Pongezi na malalamiko
Maoni yako, mazuri na mbaya, hutusaidia kukupa wewe na mtoto wako huduma bora zaidi.
Baada ya ziara yako kwa ED, utatumiwa ujumbe wa kuomba maoni yako kupitia utafiti wa MyVisit. Tafadhali kamilisha utafiti huu mfupi ili utufahamishe kuhusu uzoefu wako wa i kuhudumiwa. Unaweza kutuandikia ujumbe wa pongezi au malalamiko kupitia tovuti yetu.